Thursday, 22 December 2016

Ajari mbaya tena Shinyanga

AJALI MKOANI SHINYANGA AMBAPO BUS LA FAHARI DAR SHY LIMEGONGANA NA RAV4 NA NOAH NYINGINE KUGONGWA. AJALI HII IMETOKEA ENEO LILELILE LILILOUA WATU 21 KWWENYE NOAH.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hii waliokuwa kwenye RAV4 walikuwa wamelewa sana ndani ya gari kuna hadi chupa za castle lite, na RAV ndio iliyohama upande wake na kwenda kuipiga bus upande wa kulia.

Tuesday, 20 December 2016

2G, 3G, 4G na 5G maana yake ni nini?



 Katika sekta ya mawasiliano, ni kawaida kuwasikia wataalamu na wakati mwingine watu wa kawaida wakizungumzia kuhusu teknolojia ya 2G, 3G, 4G na 5G. Maana yake ni nini?

G kwenye tarakimu hizi inawakilisha 'Generation', yaani kizazi fulani cha teknolojia ya mawasiliano kwa kuangazia zaidi uwezo wa data kwenye simu.

Hakuna kipimo chochote kinachotumiwa kimataifa kuhusu kasi ya data ya simu.
Lakini wengi wanakubaliana kuhusu baadhi ya sifa za teknolojia hizi.

Teknolojia ya 1G, au kizazi cha kwanza cha data ya simu, ilianza kutumiwa 1991.
Teknolojia ya 2G ilianza pia kutumika katika kipindi hicho, ikiwa kama ndugu wa 1G.

Kwa 1G, ungeweza tu kupiga simu
Teknolojia hii sana ilikuwa analogu na simu za wakati huo zilikuwa kama hizi hapa chini...

 Kisha 2G ikaja na uwezo wa kutuma ujumbe mfupi au arafa
Teknolojia ya 2G ambayo pia huitwa teknolojia ya SMS iliwezesha watu kutuma ujumbe mfupi.

Ungeweza pia kutuma ujumbe wenye picha, ambao uliitwa MMS (multimedia messaging service).
Na pia simu za waka.

 Kupiga simu kwa video kuliwezekana 2001
3G na kasi yake ya data ya 2mbit/s (megabaiti 0.25 kila sekunde) ilianza kutumika wakati ambao simu za kwanza aina ya smartphone zilianza kuuzwa madukani.

Huduma yake ya mtandao haikuwa ya kasi sana lakini iliwezesha huduma ya mtandao kupatikana bila kutumia nyaya. Angalau ilikuwa hatua fulani.

Na watu waliweza kupiga simu za video.
Ili kufahamu kasi yake au mwendo wake wa upole ulivyokuwa, iwapo ungetaka kupakua filamu ya ucheshi ya David Brent: Life on the Road kutoka kwenye iTunes, ingekuchukua saa tano kupakua faili hiyo ya 4.26GB.

2010 teknolojia ya 4G ikaanza kutumika
Teknolojia hii ya kasi iliwezesha kuanza kupatikana kwa michezo mingi kwenye simu na ya kiwango cha juu.

Filamu ambayo ingekuchukua saa tano kuipakua kwa teknolojia ya 3G sasa inaweza ikakuchukua dakika 8 pekee kwa teknolojia ya 4G.

Utafiti: Betri zinazotumiwa katika simu zina sumu
Lakini 4G haipatikani maeneo yote, hata katika mataifa yaliyoendelea.
Afrika Mashariki, utaipata katika baadhi ya maeneo ya miji mikubwa.

5G ndiyo mwendo kasi?
Hii ndiyo ya kasi zaidi kwa sasa.
Tume ya Mawasiliano ya Ulaya inakadiria kwamba kati ya mwaka 2020 na 2030, utaweza kupakua filamu moja ya HD ya saa moja kwa sekunde sita pekee.

Simu za wakati huo nazo zitakuwa na muonekano gani? Kama hii hapa chini labda?


Waziri Mkuu Majaliwa Aitembelea Familia Ya Marehemu Sitta


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mama Margart Sitta, mjane wa Spika mstaafu,  Sumuel Sitta wakati alipoitembelea familia ya marehemu jijini Dar es salaam Desemba 19, 2016. Kulia ni mkewe Mary.

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kushoto  kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya aliyekuwa Spika Mstaafu, Samuel Sitta wakati walipoitembelea familia hiyo, nyumbani kwa marehemu jijini Dar es salaam Desemba 19, 2016. Kulia kwake ni mjane wa marehemu, Margareth Sitta. Wengine pichani kutoka kushoto ni watoto wa marehemu, Benjamin Sitta, John Sitta na Sam Junior.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary wakisalimiana na mama Margaret Sitta, mjane wa alieyekuwa Spika mstaafu, Samuel Sitta wakati walipoitembelea familia ya Spika huyo jijini Dar es salaam Desemba 19, 2016. Wengine pichani ni watoto wa marehemu, kutoka kushoto ni  Benjamin Sitta, Sam Junior na John Sitta.

Mazoezi ya kuondoa kitambi



Kutokuwa na kitambi ndio ndoto ya watu wengi kwa sasa wanaojali afya zao. Kutokana na kufumka kwa maradhi mbalimbali baadhi ya watu wamekuwa wakihangaika kutafuta njia rahisi za kupunguza ama kuondoa vitambi hivyo na uzito uliopitiliza.

Wapo waliamua kukaa na njaa na wengine kutumia dawa kali wakilenga kufikia malengo yao ambayo ni kupunguza uzito.

Lakini kuwa na kitambi ama ongezeko la uzito linaweza kuondolewa kwa njia rahisi sana tofauti na unavyodhani. Tena njia isiyohusisha hata chembe ya dawa itakayoweza kukuletea madhara baadaye.


Licha ya wataalamu wengi kusisitiza kuwa kitambi au ongezeko la uzito ni matokeo ya ulaji mbovu, lakini ukweli utabaki kuwa mazoezi kwa sehemu kubwa yana nafasi kubwa ya kupunguza uzito na kuondoa kitambi.

Profesa Christine Rosenbloom, mtaalamu wa lishe kutoka Chuo Kikuu cha Georgia, Marekani anasema kupunguza mafuta mwilini kunaendana na ulaji wa chakula bora pamoja na mazoezi ya kila siku.

“Unatakiwa kufanya mazoezi kwa muda usiopungua dakika 60. Kwa kufanya hivi utaweza kuondokana na matatizo ya unene ama mafuta tumbo,” anasisitiza.

Naye Profesa Michael Jensen wa Kliniki ya Mayo anasema, mazoezi ya viungo yana nafasi kubwa sana ya kuutengeneza mwili wako katika hali nzuri zaidi na pia kuufanya uwe mwepesi pia.


Ni muhimu kuelewa kuwa unapoushughulisha mwili wako, unauweka katika nafasi ya kuunguza mafuta na hivyo kujiweka kwenye nafasi ya kuondokana na unene. Ikiwa utafanya mfululizo ni wazi mwili hautakuwa na mlundikano wa mafuta.

Umuhimu wa mazoezi
Wataalamu wanasema watu wengi huamini kuwa unene ni matokeo ya kula vyakula vyenye kalori nyingi. Hivyo kwa kupunguza kalori wanaamini kuwa itakuwa ni njia rahisi ya kupunguza uzito wa mwili.


Licha ya kuamini hivyo lakini wataalamu wanasisitiza kufanywa kwa mazoezi kwani ndiyo njia pekee itakayoufanya mwili wako kukubaliana na mpango mzima wa kupunguza hizo kalori huku ukiipa nafasi misuli yako kuurudisha mwili katika hali inayotakiwa.

Wanasema kupunguza kalori kwa njia isiyokuwa na mazoezi huwaweka wahusika katika hali ya kunenepa zaidi endapo ataamua kurudi katika ulaji wake wa kawaida.


Kujenga misuli
Jambo la muhimu unalopaswa kufahamu unapoamua kuanza mpango wa kupunguza uzito na mafuta mwilini ni kujua ni nini hasa unatakiwa kufanya. Kuwa na malengo ndiyo jambo la msingi litakalokusaidia kukutia nguvu na hata kufanikiwa.

Watafiti kutoka maabara ya Chuo Kikuu cha San Diego Marekani, waliunganisha mazoezi mbalimbali ya tumbo. Matokeo yake waligundua kuwa mazoezi ya tumbo yana nafasi kubwa sana ya kuikaza misuli inayozunguka tumbo na hivyo kurahisisha zoezi la kupunguza kitambi na kulifanya tumbo kuwa bapa.

Yafuatayo ni mazoezi matano muhimu katika kupunguza mafuta tumboni:


Zoezi la baiskeli –
Hili husaidia kukata tumbo sehemu ya chini na ya juu. Unachotakiwa kufanya ni kulala chali. Kisha chukua mikono shika kichwani kwa nyuma upande wa kisogoni. Wakati umelala kunja miguu yako na kisha jinyanyue hadi kujikunja mfano wa ‘c’ iliyolalia mgongo. Fanya hivyo mara 12 hadi 16.


Zoezi la “Sit ups’
Ukiwa umelala chini. Nyoosha miguu yako. Kisha nyoosha juu mikono yako. Jinyanyue na kugusa miguu yako. Fanya hivyo mara 20 hadi 30.


Zoezi la kunyoosha tumbo
Kaa chini na nyoosha miguu yako huku ukiitanua hadi kufikia uwezo wako wa mwisho. Geuza kifua chako hadi uweze kuona upande wa nyuma yako kwa uzuri zaidi bila kugeuka mwili mzima. Fanya hivyo huku ukibadilisha upande. Hakikisha unafanya mara 10 kwa kila upande, mkono wako wa kulia uweze kuzunguka.


Zoezi kunyonga miguu
Hili ni maalumu kwa ajili ya tumbo la chini. Lala chali na kisha nyanyua miguu yako. Anza kuinyonga kama unavyofanya unapoendesha baiskeli. Fanya hivyo mara 20. Utasikia maumivu katika tumbo lako la chini.


Zoezi la kuzungusha kiuno
Simama na kisha shika mikono yako kiunoni. Tanua miguu yako ili kusimama imara. Zungusha mwili wako kuanzia kwenye kiuno kuja juu huku ukiwa umesimama bila kugeuka.

Mwakyembe ampongeza Makonda


WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kitendo chake cha kuwasaidia wananchi wa mkoa huo kupata huduma za msaada wa kisheria na mpango wa kujenga mahakama 20 mpya.

Dk Mwakyembe ametoa pongezi hizo jana alipokutana na Makonda ofisini kwake jijini Dar es Salaam wakati viongozi wa wizara hiyo walipomtembelea kumpongeza na kuunga mkono jitihada zake katika kuhakikisha wananchi wa Dar es Salaam wanapata haki zao kwa wakati.

“Mkuu wa Mkoa nimekuja hapa hii leo (juzi) na timu yangu kukupongeza na kukuonesha kwamba tunakuunga mkono na tuko pamoja kuhakikisha upatikanaji haki na huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi vinapatikana kwa wakati,” amesema Dk Mwakyembe.

Akizungumza katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Sifuni Mchome alisema wizara imenufaika na ziara ya Makonda ambayo ilimpatia fursa ya kusikiliza kero, malalamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi na kuonesha kuwa wananchi wengi wanahitaji msaada wa huduma za kisheria ili kupata haki zao kwa wakati.

Makonda akizungumza katika kikao hicho, alisema uongozi wa mkoa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wanatarajia kujenga mahakama mpya 20 kuanzia mwaka 2017, kukabiliana na upungufu wa mahakama mkoani humo kwa kuwa mkoa una mahakama za mwanzo 12 wakati mahitaji halisi ni mahakama 102.

Makonda amesema uamuzi wa kujenga mahakama hizo unaenda sambamba na mpango wa kujenga vituo vya polisi katika kila kata ambao ulisaidia kugundua kuwa ili haki itendeke tena kwa wakati kwa wananchi watakaopelekwa katika vituo hivyo vya polisi, ni lazima kuwe na mahakama.

Amesema ziara aliyoifanya mkoani hivi karibuni ilimpatia fursa ya kusikiliza kero za wananchi na kugundua kuwa wananchi wengi wanakabiliwa na tatizo la kutopata haki kwa wakati, uelewa mdogo wa namna ya kupata haki zao hali ambayo inawasababisha wengi wao kukosa haki zao kwa wakati.

Amesema mpaka sasa anao vijana 35 ambao ni wahitimu wa shahada ya sheria ambao wamepatiwa mafunzo maalum na mwanasheria wa mkoa na atawasambaza vijana hao katika wilaya zote za mkoa ili kuwahudumia wananchi kwa kuwapatia msaada wa huduma za kisheria.

Lema kuendelea kukaa rumande


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha imeruhusu maombi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kukata rufaa ya kuomba dhamana yake ndani ya siku 10 kuanzia jana. Wakati mahakama hiyo ikiruhusu hilo, tayari mawakili wa Lema wamesajili rufaa namba 126/2016 katika mahakama hiyo jana jioni.

Awali akizungumza kuhusu ruhusa hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Dk Modesta Opiyo alisema hakukuwa na ucheleweshwaji wowote wala ukiukwaji wa sheria kwa mawakili wa Lema, walioufanya wakati wa uwasilishaji wa maombi ya kuongezewa muda wa kukata rufaa.

Akisoma uamuzi wa kama maombi hayo ya Lema yalikuwa ndani ya muda au la, Jaji Opiyo alisema maombi hayo yalikuwa ndani ya muda kwa sababu mawakili wa serikali walihesabu siku hadi za mwisho wa wiki (Jumamosi na Jumapili).

Alisema hakukuwa na uvunjaji wa sheria, uliofanywa na mawakili wa mbunge huyo, bali mawakili wa serikali wao waliweka pingamizi zao wakahesabu hadi siku za mapumziko.

"Mahakama hii imemruhusu Lema kukata rufaa ndani ya siku kumi kuanzia leo hii, pia busara ya mahakama ni lazima iangaliwe katika kuamua jambo hili la uamuzi wa rufaa hii, hivyo mawakili wa Lema hawakuwa nje ya muda kama ilivyodaiwa na mawakili wa serikali," alisema.

Akichambua hoja za mabishano ya kama nia ya notisi ya kukata rufaa ilipitiliza muda wake au la Jaji Opiyo, alisema awali alitupilia mbali pingamizi wiki iliyopita baada ya kupitia hoja za pande zote.

Alisema kuwa pingamizi hizo za serikali, walizokuwa wakitaka maombi hayo yasisikilizwe kuwa mawakili hao hawakuwa na hoja za kisheria zenye mashiko.

Maombi hayo namba 69, upande wa serikali ulikuwa ukiwakilishwa na Wakili Hashim Ngole, Matenus Marandu, Elizabeth Swai na Adelaide Kasala huku Lema akitetewa na wakili, Sheck Mfinanga na Faraji Mangula.

Akiwasilisha hoja za maombi ya kuongezewa muda wa kuwasilisha notisi hiyo ili rufaa hiyo iweze kusikilizwa, Wakili Mfinanga alidai mahakamani hapo kuwa maombi hayo, yamewasilishwa mahakamani hapo chini ya Kifungu 361(2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Alidai kuwa maamuzi wanayotarajia kukatia rufaa ni uamuzi uliotolewa Novemba 11 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na Hakimu Desderi Kamugisha, ambapo Lema anakabiliwa na kesi namba 440 na 441 za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.

Alitaja sababu mbili za msingi za kukatia maamuzi hayo rufaa kuwa ni kuiomba mahakama hiyo, ipitie makosa ya kisheria yaliyofanywa na mahakama ya chini.

Alisema kuwa uamuzi huo, ulimpa mleta maombi (Lema) dhamana, ila kabla hajapewa masharti ya dhamana, upande wa Jamhuri ulitoa notisi ya nia ya kukata rufaa. Alidai mahakamani hapo kuwa wanaiomba mahakama hiyo, iwape muda ambao hautazidi saa 1:30 kwa ajili ya kuleta notisi hiyo ili mahakama iweze kurekebisha makosa hayo, yaliyofanyika na mahakama ya chini.

Akiwasilisha hoja ya pili, Wakili Mangula alidai mahakamani hapo kuwa tangu kutolewa kwa uamuzi huo, hawakuwa wamepumzika, muda wote walikuwa mahakamani na walikuwa wanakuja kwa njia tofauti ili kuiomba mahakama irekebishe makosa hayo ya kisheria.

Alisema baada ya uamuzi huo kutolewa, muda wa kazi ulishaisha na ilikuwa siku ya ijumaa, hivyo Novemba 14 mwaka huu walipeleka barua ya malalamiko mahakamani hapo. Walipoitwa pande zote mbili katika shauri namba 6, walikumbana na pingamizi zilizowasilishwa na mawakili wa serikali.

Akijibu hoja za waleta maombi hao, Wakili Ngole alidai kuwa ni wazembe na kuwa hata uamuzi wanaolalamikia mahakamani hapo.

Awali ulimpa mleta maombi dhamana, lakini kabla hajapewa masharti ya dhamana, mahakama iliingiliwa mamlaka yake na hawajawasilisha maombi hayo.

Wakili huyo alidai mahakamani hapo kuwa hakukuwa na makosa yoyote ya kisheria, kama inavyodaiwa na waleta maombi hao na kudai kuwa baada ya hakimu kusema mahakama inampa mshitakiwa dhamana, Jamhuri kwa haki yake, walisimama na kuifahamisha mahakama wana nia ya kukata rufaa.

Baada ya Jaji Opiyo kutoa uamuzi huo, mawakili wa Lema wakiongozwa na Mfinanga pamoja James Millya, waliweza kuwasilisha mahakamani nia yao ya kukata rufaa na ilipokelewa mahakamani hapo. Inasubiri tarehe ya kupangiwa Jaji pamoja kusikiliza kwa dharura na hatimaye Jaji huyo atakayepangiwa, kuamua kama apate dhamana au la.

Nje ya mahakama, watu mbalimbali waliohudhuria kesi hiyo walikuwa na furaha huku wakikumbatiana, wakiwemo ndugu wa Mbunge huyo. Lema alirudishwa mahabusu iliyopo Gereza la Kisongo kwa ajili ya kusubiri kuwa nje kwa dhamana au la.

Lema alikamatwa Novemba 2, mwaka huu nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma, ambapo alifikishwa mahakamani Novemba 8, mwaka huu akikabiliwa na mashitaka ya uchochezi ikiwemo kumtukana Rais John Magufuli. Mawakili wa Lema walidai kuwa tayari jana jioni wamesajili rufaa hiyo namba 126 ya mwaka 2016.

MAGAZETI YA LEO 21 / 12 / 2016































Ufafanuzi wa Simba kuhusu kupokwa pointi za Ndanda


Baada ya ushindi wa Simba 2-0 Ndanda, kuwa na taarifa zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii kwamba huenda Simba ikapokwa pointi kwa kosa la kuwachezesha wachezaji wawili wa kigeni (Daniel Agyei na James Kotei wote kutoka Ghana) ambao bado hawajakamilisha vibali vya kufanyia kazi nchini.

“Niseme hizo taarifa ni za uzushi ambazo zimeletwa na wapinzani wetu ambao waliamini kwamba tutapoteza mchezo wetu dhidi ya Ndanda na wao wataendelea kuwa juu ya msimamo wa ligi kwa hiyo ushindi wetu haujawapendaza ndio maana wameamua kuendesha vita ya maneno ya uongo na uchochezi,” amenukuliwa makamu wa rais wa Simba SC Geoffrey Nyange Kaburu wakati akizungumza kwenye kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM.

“Simba imekamilisha taratibu zote za usajili ambazo zipo ndani ya kanuni zetu za VPL, baada ya kukidhi mahitaji yote wachezaji husika walipewa leseni na TFF na ndio ambazo zilitumiwa siku ya mchezo kwa hiyo vijana wetu walikuwa na vigezo vyote vya kucheza dhidi ya Ndanda kulingana na kanuni zetu.”

“Wanachama na wapenzi wa Simba wapuuzie haya maneno, kwa sasa lengo letu ni kwenye mchezo wetu unaofata dhidi ya JKT Ruvu siku ya Jumamosi na kubwa ni kuendelea kuvuna pointi na hilo ndio kiu ya wengi kuona timu inashinda kila mechi na hatimaye kutwaa ubingwa.”

Viongozi wapya CCM waja na Tanzania mpya

Viongozi wapya wa CCM wameeleza fikra na mipango ya awali na namna walivyojipanga, kusimamia na kutekeleza ajenda ya mageuzi ndani ya chama hicho ambayo msingi wake ni kuirejesha CCM kwa watu

Viongozi hao wapya ambao leo wamekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa chama hicho Dkt. John Magufuli Ikulu Dar es Salaam, ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu Bara Bw. Rodrick Mpogolo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi Bw. Humphrey Polepole na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Siasa na Mambo ya Nje Kanali Mstaafu Ngemela Eslom Lubinga.

 

Baada ya mazungumzo hayo, Polepole amesema Na Mhe. Rais ametuhakikishia kwa asilimia 100 kwamba msimamo wa kufanya mageuzi kwenye Chama Cha Mapinduzi, kukirudisha kwenye misingi ambayo chama hiki kilianzishwa, yaani chama cha wanyonge na chama ambacho kinajinasibu na shida za watu, unatekelezwa.

"Ametuambia tukafanye kazi kwa bidii, Watanzania wana matumaini makubwa sana na Chama Cha Mapinduzi na sisi tumemhakikisha kwenda kuchapa kazi ili dhamira ya kujenga Tanzania mpya iweze kuakisiwa na kuletwa na CCM Mpya" amesema Bw. Polepole.

Watu 20 wauawa katika maandamano  DR Congo 


 Waandamanaji 20 wameuawa na wanajeshi katika mji mkuu wa DR Congo Kinshasa ,kulingana na mtandao wa polico.cd nchini humo.

Watu wengine watano walijeruhiwa, wawili vibaya baada ya kupigwa risasi wakiwa karibu na maafisa wa kikosi cha Republican Guard katika mji wa N'djili mojawapo ya wilaya zenye idadi kubwa ya watu.

Milio ya risasi bado inaendelea kusikika katika maeneo tofauti mji Kinshasa, licha ya kuwa kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi ametaka kufanyika kwa maandamano ya amani, ripoti hiyo imeongezea.

Maandamano yamekuwa yakifanyika katika miji kadhaa ya DR Congo ambapo muhula wa rais Joseph Kabila uliisha siku ya Jumatatu.

Wakati huohuo kumekuwa na maandamano katika miji kadhaa mikuu duniani ya kumtaka rais wa DR Congo Joseph Kabila kujiuzulu.

Mapema siku ya Jumanne milio ya risasi iliendelea kusikika huku waandamanaji wakimtaka rais Kabila kujiuzulu.

Raia bado wanaendelea kupiga firimbi mjini Kinshasa.

Wanasema kuwa hatua hiyo inatoa ishara kwamba muhula wa Kabila umekamilika.

Pia wanaimba kwamba Kabila Must Go { kabila ni sharti aondoke mamlakani}, kulingana na ripoti za BBC

KUNA WIZI UMETOKEA BENKI


••••••••••••••• •••••••
Jambazi akasema "wote laleni chini pesa
ni za serikali na maisha ni ya kwenu",
wote wakalala chini (HII INAITWA
DHANA ...YA USHAWISHI - kubadilisha
njia ya
kawaida ya kufikiria)
••••••••••••••• •••••••
Kuna dada kwa woga akawa
amelala chini kimitego, Jambazi
akamwambia, "dada hebu kuwa
na adabu chukua kanga jifunike hili ni
tukio la ujambazi na sio la
ubakaji.” (HUU UNAITWA WELEDI -
zingatia ulichofundishwa kufanya)
••••••••••••••• ••••••••
Walipotoka kwenye
wizi jambazi mdogo ambaye ana shahada
ya uzamili ya biashara akamwambia
mwenzake, "tuzihesabu hizi fedha.” Yule
mkubwa akamcheka
kwa dharau na kumjibu, "wewe
mjinga sana hizo hazina haja ya
kuhesabu saa mbili wata tutangazia
kwenye taarifa ya habari tumeiba kiasi
gani. (HUU INAITWA UJUZI - Siku hizi
ujuzi ndio bora kuliko vyeti)
•••••••••••••••••••••••
Baada ya majambazi
kuondoka meneja akamwambia mhasibu
wa bank, " ujumlishie na zile milioni 80
tulizo iba sisi.” (HUKU KUNAITWA
KUOGELEA NA MKONDO WA MAJI -
kushabihiana na mazingira magumu kwa
faida binafsi.)
••••••••••••••• ••••••••
Mhasibu akafurahi na kusema, "dah wizi
ukitokea kila mwezi itakuwa burudani
sana.” (HUKU KUNAITWA KUWA NA
MAWAZO CHANYA - Furaha ndio kitu cha
muhimu zaidi)
••••••••••••••••••••••
Meneja kafurahi sana
kwa kuwa sasa matatizo yake
yametatuliwa
na wizi uliojitokeza. (HUKU KUNAITWA
KUTHUBUTU-shiki lia nafasi pale
inapojitokeza hata kama ni hatari kiasi
gani.
••••••••••••••• ••••••••
Haya usiku wake
taarifa ya habari
ikatangaza kuwa wizi mkubwa sana wa
million 100 umetokea leo benki.
Majambazi kuskia hivyo wakaanza
kuhesabu zile pesa lakini wakajikuta na
milioni 20 tu.
Yule jambazi mkubwa akashtuka na
kusema, "dah! yaani meneja kaiba mara
nne zaidi yetu bila kuchezesha msuli?
Bora umeneja kuliko ujambazi.” (HII
INAITWA
ELIMU NDIYO KILA KITU - ishike sana
elimu ina nguvu kuliko chochote.)

MAMBO KUMI MAGUMU YA KUFAHAMU KUHUSU WANAWAKE....


1. Mwanamke ni kama Shule, kamwe hauwezi hitimu.
2. Mwanamke anahitaji matunzo na kujaliwa, usipofanya hivyo unakaribisha wengine kufanya hayo.
3. Cheti chako cha ndoa yako na yeye sio "leseni ya udereva" ni "kibali cha kujifunza"
4. Inachukua muda kidogo mwanamke kukuamini, ni vigumu kumbadili akikuamini, ila ukijichanganya tu, msahau! Hawezi kukuamini tena.
5. Anaweza akawa mwiba mchungu au Malaika mwenye baraka, inategemeana na jinsi unavoishi nae.
6. Ni vigumu mwanamke kusahau vitu, hukumbuka mambo yaliyopita kirahisi na hii huwaumiza sana, jizuie usimuumize.
7. Wanawake huhitaji sana kuongea pale wanapokuwa too emotional (wakiwa wamekasirika au wameudhiwa). Wanapoona mwanaume hautaki kumsikiliza, huenda na kulia kwa marafiki zao wa karibu.
8. Wanawake wanapenda sana kuombwa msamaha! anapenda msamaha mara nyingi zaidi kuliko hata anavyompenda mwanaume wake.
9. Mwanamke anapokuwa na hasira, takribani nusu anayoyazungumza ni kinyume chake na hayamaanishi.
10. Wakati mgumu sana kwa mwanamke, ni wakati ambao yupo mbali na mwanaume anaempenda kwa dhati. Sio mbali kimwili tu. Hata kihisia pia.
Nitaendelea na TIPS za upande wa wanaume muda mwingine...msichoke na darasa!
"Love is magic when you understand our differences, and women are beautiful part of God's creation, you will enjoy if you understand her. Use your brain and ask for God's guidance!"
Siku Njema...

Wahitimu udaktari kupelekwa vituo vya afya


WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema inakusudia kuwasilisha muswada wa sheria bungeni mwakani, itakayowalazimisha wahitimu wa udaktari kupangiwa kwenye kituo chochote cha afya na Serikali, ambako watafanya kazi katika kipindi kisichopungua miaka miwili.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk Hamis Kigwangalla huenda muswada huo, ukawasilishwa rasmi katika Bunge la Februari mwakani.

Dk Kigwangalla aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya sekta ya afya katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wa serikali ya awamu ya tano na mikakati ya kuboresha zaidi sekta hiyo katika miaka ijayo.

Alisema endapo sheria hiyo mpya itapitishwa na bunge hilo, inakusudia kubadili muundo mzima wa watumishi wa sekta ya afya.

“Sheria hii, itaweka kipindi cha lazima cha national service (utumishi wa umma) na kila daktari anayehitimu kwa sababu amesomeshwa na kodi za watanzania, atalazimika kupangiwa kwenye kituo chochote cha serikali ambako atafanya kazi kwa kipindi kisichopungua miaka miwili kwa lazima”.

Naibu waziri huyo, alisema katika mipango na matarajio ya wizara hiyo kwa mwaka ujao wa 2017, pia wanatarajia kutunga sheria ya kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na bima ya afya ya lazima.

Alisema katika kutekeleza azma hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja, serikali imefanikiwa kuwakatia bima wazee wote waliopo nchini wanaokadiriwa kufikia takribani milioni mbili na nusu.

“Bado utaratibu huu wa kuwakatia bima unaendelea katika halmashauri zingine, lakini tunakoelekea tunaweka sheria ili jambo hili lisiwe tu ni agizo la serikali bali litambulike na kutekelezwa kisheria,” alisisitiza Dk Kigwangalla.

Alisema katika sheria hiyo mpya kutakuwa na kifungu cha sheria kitakachobainisha makundi yote yanayotakiwa kukatiwa bima kwa usimamizi wa halmashauri zao.

Aidha Dk Kigwangalla alisema pia wizara hiyo ina mpango wa kuhakikisha inarasimisha suala la matibabu bure kwa makundi maalumu kwa kulitambua kisheria, ili liweze kutekelezwa na kuwafikia walengwa.

Alisema kwa mujibu wa sera ya afya ya taifa, wazee wote wenye miaka zaidi ya 60, watoto wenye umri chini ya miaka mitano pamoja na watu wenye magonjwa sugu kama vile saratani, shinikizo la damu, sukari na pumu wanapaswa kupata huduma bure.

“Jambo hili lipo na linatambulika kisera, lakini leo hii bado makundi haya yanaishia kuwaona madaktari bure lakini wanalipia dawa na wakati mwingine huduma, tutakapoingia na kutunga sheria hii mpya mwakani, hili litakuwa jambo la kisheria, na tutasimamia utekelezaji wa sheria hiyo,” alisisitiza.

Akizungumzia mipango ya wizara hiyo chini ya usimamizi wa serikali ya awamu ya tano, naibu waziri huyo alisema, wizara hiyo imejipanga kuboresha zaidi huduma za afya, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha huduma za afya zinafika hadi vijijini.

Alisema katika kipindi cha awamu ya kwanza ya serikali ya awamu ya tano wizara ya afya, imejipanga kuhakikisha inaongeza vituo vya afya kutoka 489 vilivyopo hadi kufikia vituo vya 1,000 ambavyo vyote au kwa asilimia kubwa vitakuwa pia vinatoa huduma muhimu za upasuaji kwa akinamama na upasuaji wa dharura.

“Kwa mwaka unaokuja matarajio yetu ni kuhakikisha tunaongeza idadi ya vituo vya afya vinavyotoa huduma za upasuaji kwa wajawazito, lakini pia ni lazima kuwe na huduma za uchunguzi wa magonjwa kupitia maabara na huduma za upasuaji,” alifafanua.

Alisema kupitia mpango huo, serikali itajenga timu za upasuaji katika kila kata zitakazokuwa na wataalamu wa kila fani inayotumika katika upasuaji, kuanzia fani ya usingizi, uuguzi katika vyumba vya upasuaji na madaktari wa upasuaji.

“Kwa sasa kuna vituo vya afya 489 na vilivyokuwa vinatoa huduma ya upasuaji ni vituo 113 sasa tunataka vituo vyote vitoe huduma hiyo kwa akinamama na upsuaji wa dharura,” alisisitiza.

Alisema tayari katika mwaka ujao, wizara hiyo imeilekeza mikoa na wilaya zote kutenga angalau kituo kimoja na kukiingiza kwenye bajeti itakayokuja mwakani, ili kuongeza idadi ya vituo vya afya vifikie hadi 700. Pamoja na hayo naibu huyo waziri alibainisha kuwa katika mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa serikali ya awamu ya tano katika sekta ya afya, kumekuwa na mafanikio makubwa katika sekta hiyo, ikiwemo kuboreshwa kwa huduma za afya na upatikanaji wa vipimo na tiba.

“Katika awamu hii, viongozi wakuu wamekuwa wakifuatilia kwa karibu maendeleo ya sekta ya afya, hata Rais John Magufuli mwenyewe alifanya ziara kadhaa katika hospitali kubwa ikiwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) hali iliyochangia kuimarika kwa kasi kwa sekta hiyo ya afya,” alisema.

Oktoba mwaka huu, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella Manyanya alisema serikali iko katika mkakati wa kuwabana wanafunzi wanaopewa mikopo katika fani za kipaumbele, wanapohitimu masomo yao, kutumikia katika utumishi wa umma nchini kwa muda fulani ili kuhakikisha dhamira ya serikali ya kuwapa kipaumbele inatimia.

Fani hizo ni sayansi za tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati, uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo, mafuta, gesi asilia, sayansi asilia, mabadiliko ya tabianchi, sayansi za ardhi, usanifu majengo na miundombinu.

Hatua hiyo inatokana na serikali kubaini kuwapo wanafunzi wanaosomea fani hizo ili kupata mikopo, lakini baada ya kumaliza hukimbilia kufanya kazi nyingine au nje ya nchi, hivyo upungufu wa wataalamu waliowakusudia kubaki kama ilivyo.