Mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva amesema hamfikirii mchezaji anayeongoza katika orodha ya wafungaji bora, anachofikiria yeye ni timu yake kupata matokeo uwanjani.
Msuva ameyasema akiwa tayari amefikisha mabao 9 baada ya kufunga magoli mawili kwenye mchezo wa Jumamosi dhidi ya JKT Ruvu ambayo yamemwezesha kumfikia Shiza Kichuya wa Simba na wote wanamagoli tisa hadi sasa.
“Simfikirii mtu ambaye anaongoza kwa magoli au haongozi kwa magoli, nachofikiria mimi ni timu yangu na mimi nifanye nini katika timu ipate faida kwani kazi yangu ya kwanza ni kutengeneza nafasi, kazi ya pili ni kufunga ,” amesema .
Msuva amesema, Ligi ina ushindani mkubwa lakini kwa upande wao wanajitahidi kuweza kutetea Ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment